Lugha Nyingine
Mkutano wa Kutangaza shughuli za utalii za Eneo Kubwa la Mlima Huangshan wafanyika Beijing (10)
Li Peisheng na Hu Xiaochun wenye sifa ya “watu wema wa China” wanasimulia mvuto wa “Eneo Kubwa la Mlima Huangshan”. |
Tarehe 23, Agosti, mkutano wa kutangaza kwa Dunia shughuli za utalii za Eneo Kubwa la Mlima Huangshan ulioandaliwa na Idara ya Utamaduni na Utalii ya Mkoa wa Anhui na Ofisi ya Mawasiliano ya Habari za Intaneti ya kamati ya chama ya Mkoa wa Anhui ulifanyika katika shirika la Gazeti la Umma.
Mlima Huangshan unajulikana nchini na nje ya China kutokana na mandhari yake nzuri. Ukiwa ni mali za dunia za urithi wa mazingira ya asili na wa kiutamaduni, mlima huo ni chimbuko la shughuli za utalii kwa hivi sasa nchini China.
Kutokana na mlima maarufu wa Huangshan, Mkoa wa Anhui umeanzisha shughuli za utalii kwenye “Eneo Kubwa la Mlima Huangshan” linalohusisha miji minne ya Huangshan, Chizhou, Anqing na Xuancheng na wilaya 28.
Mkutano huo wa kutangaza shughuli za utalii uliwaalika wawakilishi wa sekta nane kuwa watangazaji wa shughuli za utalii za “Eneo Kubwa la Mlima Huangshan”, ambao walisimulia vilivyo mvuto wa eneo hilo kwa kupitia walivyojionea.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma