Lugha Nyingine
Ghala la Nafaka la Xizang Lakaribisha Mavuno Mazuri
Picha ikionyesha hali ya mavuno ya vuli katika Mji mdogo wa Baza, Wilaya ya Bailang, Mji wa Shigatse, Mkoa wa Xizang, Septemba 10 (picha kwa droni). (Xinhua/Jigme Dorje) |
Katika msimu wa mavuno, mashamba ya Shigatse, yanayojulikana kama "Ghala la Xizang", yamekuwa rangi ya njano ya dhahabu. Wakulima wametumia njia za mashine na nusu-mashine kuvuna shayiri kwa ufanisi.
Mji mdogo wa Baza ulianzisha ushirika mwaka 2014 na kunufaisha wakulima 846 wa sehemu hiyo. Sio tu wanakijiji wamepata fursa ya kutumia mashine za kilimo za ushirika, bali pia wamepokea gawio la maelfu ya Yuan kila mwaka. Mashine hizi za kisasa za kilimo zimeinua ufanisi wa kuvuna shayiri na kupunguza kazi kwa wanakijiji.
Pamoja na kutumia mashine, ushirika umelima aina mpya za shayiri kama vile "Shayiri ya Xizang 2000", "Shayiri ya Xizang 3000" na " Shairi ya Himalaya 22". Aina hizi za shayiri zenye sifa bora zimekidhi mahitaji ya soko la Xizang, pia zimeuzwa kwa Gansu, Qinghai, Sichuan, Yunnan na maeneo mengine. Mwaka huu, mauzo ya mbegu bora za shayiri ya ushirika wa Kijiji hicho yalifikia kilo milioni 1.58115, na thamani ya mauzo imefikia yuani milioni 11.4.
Maendelo ya mji mdogo wa Baza ni alama ya mchakato wa kilimo cha kisasa wa Xizang. Kutokana na takwimu ya Idara ya Kilimo na Masuala ya Vijijini ya Mkoa wa Xizang imeonyesha kuwa mwaka 2023, mavuno ya shayiri ya Xizang yalifikia tani 843,600, maeneo ya upandaji yalifikia mu 2,228,700(takriban hekta 148,580), na mashamba ya kiwango cha juu yalifikia mu milioni 4.3(takriban hekta 287,000), maeneo ya upandaji wa shayiri yenye sifa bora yalifikia 93% na kiwango cha mavuno na upandaji wa mazao makuu ya chakula kwa mashine kimefikia zaidi ya 71%.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma