超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Mjumbe wa China aitaka Israel kukomesha mara moja uwepo wake?kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 18, 2024

Fu Cong, mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, akizungumza wakati wa kikao maalum cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 17, 2024. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA - Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Fu Cong siku ya Jumanne katika kikao maalum cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina ametoa wito kwa Israel kuitikia mwito mkali wa jumuiya ya kimataifa kwa kukomesha mara moja uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Katika hotuba yake, Balozi Fu amesema miongo kadhaa ya uvamizi na ukandamizaji imesababisha mateso yasiyoelezeka kwa watu wa Palestina, na kuifanya ndoto ya muda mrefu ya kuwa na nchi huru iwe ngumu zaidi.

"Kukomesha kukaliwa huko kwa mabavu siyo chaguo, bali ni wajibu wa kisheria kwa Israeli," amesisitiza.

Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), katika maoni yake ya ushauri yaliyotolewa Julai 19, ilihitimisha kidhahiri kwamba Israel kuendelea kuwepo katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu inakiuka sheria za kimataifa, na kwamba Israel ina wajibu wa kukomesha mara moja uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, balozi huyo amesema, akiongeza kuwa maoni ya ushauri ya ICJ yanathibitisha makubaliano ya muda mrefu ya jumuiya ya kimataifa na kubainisha kiini cha suala la Palestina.

"Tunaitaka Israel kutii mwito mkali wa jumuiya ya kimataifa kwa kukomesha mara moja uwepo wake kinyume cha sheria katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu," amesema.

Balozi Fu amesema kuwa kukomesha ukaliaji huo kimabavu wa Israel ni kurekebisha dhuluma ya kihistoria na, kimuhimu zaidi, kuweka msingi wa amani.

Akisisitiza kuwa na nchi huru ni haki isiyoweza kuwa na mbadala ya watu wa Palestina kama taifa, balozi huyo amesema ukaliaji huo haramu wa kimabavu wa muda mrefu umezuia kufikia kujitawala kwa watu wa Palestina na kuipa Israel kura ya turufu ya kipekee dhidi ya Palestina. "Hii haikubaliki."

Balozi Fu amesisitiza kuwa, kutekeleza suluhu ya nchi mbili ndiyo njia pekee inayoweza kutatua suala la Palestina, na ni maafikiano ya jumuiya ya kimataifa.

Fu Cong, mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, akizungumza wakati wa kikao maalum cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 17, 2024. (Xinhua/Xie E)

Fu Cong, mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, akizungumza wakati wa kikao maalum cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 17, 2024. (Xinhua/Xie E)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha