超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Barabara Kuu ya Nairobi iliyojengwa na Kampuni ya China yateuliwa kuwania tuzo ya uvumbuzi bora wa kiteknolojia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 19, 2024

NAIROBI - Barabara Kuu ya Nairobi (Nairobi Expressway) iliyojengwa na kampuni ya China nchini Kenya imeteuliwa kuwania kipengele cha "Uvumbuzi Bora wa Kiteknolojia katika Usafiri" kwenye Tuzo za Usafiri za Afrika Mashariki Mwaka 2024, taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano imesema.

"Nairobi Expressway inawania kipengele cha Ubunifu Bora wa Kiteknolojia katika Usafiri kwenye Tuzo za Usafiri za Afrika Mashariki 2024, na tunahitaji kura yako. Tupigie kura leo na utusaidie kuendelea kuleta mapinduzi ya usafiri nchini Kenya," imesema Moja Expressway, kampuni ya China inayoendesha barabara hiyo.

Tuzo za Usafiri za Afrika Mashariki zinasherehekea ubora katika sekta ya usafiri Afrika Mashariki, zikikutanisha pamoja kampuni za kibinafsi pamoja na mashirika mbalimbali ya serikali, amesema mratibu wa tuzo hizo.

Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa Nairobi Expressway kuteuliwa kwenye tuzo hizo. Mwaka 2023, ilishinda tuzo katika vipengele vya "Muundombinu Bora wa Usafiri" na "Usafiri Endelevu" kwenye tuzo za mwanzo kabisa.

Barabara hiyo kuu iliyojengwa na Kampuni ya China imefungua fursa mpya kwa waendeshaji mabasi ya abiria ya masafa mafupi mjini na kupunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kusafiri kwa abiria na madereva. Moja Expressway pia imeeleza kuwa magari zaidi ya 70,000 hutumia barabara hiyo kila siku.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha