Lugha Nyingine
Serikali ya China hairuhusu kamwe shughuli zozote haramu au za?mabavu : Msemaji wa Mambo?ya Nje
BEIJING - Serikali ya China hairuhusu kamwe shughuli zozote haramu au za mabavu, na China imekuwa na itaendelea kuchukua hatua madhubuti kulinda usalama wa raia wote wa kigeni nchini China, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema Alhamisi.
Lin amesema hayo alipoulizwa na kutoa maoni yake kwamba ubalozi mdogo wa Japan mjini Guangzhou umetoa habari siku ya Alhamisi, ukisema kwamba mvulana wa shule aliyechomwa kisu huko Shenzhen amefariki dunia siku ya Jumatano.
"Tunasikitika na kuhuzunishwa na tukio hili la kusikitisha. Tunaomboleza kuondokewa na mvulana huyo na nyoyo zetu zinaenda kwa familia yake," Lin amesema.
Kijana huyo mdogo ni raia wa Japan, na baba yake na mama yake ni raia wa Japan na raia wa China mtawalia. Baada ya shambulio hilo, kijana huyo alipelekwa hospitali mara moja, na Mkoa wa Guangdong ulituma wataalam wa matibabu kumwokoa kwa juhudi zote, Lin amesema, akiongeza kuwa upande wa China utatoa msaada unaohitajika kwa familia yake katika kushughulikia mambo yanayohusika.
Tukio hilo bado linachunguzwa na mamlaka husika ya China italishughulikia kwa mujibu wa sheria, Lin amesem
"Kwa mujibu wa kile tunachojua hadi sasa, hili ni tukio moja la kakwaida, tukio kama hilo linaweza kutokea katika nchi yoyote. China inasimamia inalinda utekelezaji wa sheria. Serikali ya China kamwe hairuhusu shughuli zozote haramu au za kimabavu vurugu na itafanya uchunguzi wa kesi hiyo na kumwadhibu mtenda jinai kwa mujibu wa sheria," Lin amesema.
"Tunaamini kesi za watu binafsi hazitaathiri mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Japan," Lin ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma