超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Zaidi ya watu 342,000 wakimbia makazi yao nchini Somalia ndani ya miezi 8

(CRI Online) Septemba 23, 2024

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema, mapigano, ukosefu wa usalama na mabadiliko ya tabianchi yamefanya watu zaidi ya 342,000 kuwa wakimbizi wa ndani nchini Somalia.

Mtandao wa Ulinzi na Usimamizi ulio chini ya Shirika hilo umesema, watu 23,000 wamekosa makazi mwezi Agosti pekee, huku asilimia 43 ya watu hao ikitokana na mapigano, ukosefu wa usalama, mafuriko ama ukame.

Katika ripoti yake ya kazi iliyotolewa mjini Mogadishu, UNHCR imesema, mahitaji ya dharura kwa watu hao ni chakula, makazi, maji na huduma za afya, na kutaja majimbo ya Bari, Juba ya Kati, Gedo na Lower Juba kuwa majimbo yaliyopokea wakimbizi wengi wa ndani.

Kwa mujibu wa UNHCR, wanawake na watoto ambao ni kundi lililo hatarini zaidi, wanachukua asilimia 80 ya idadi ya jumla ya wakimbizi hao wa ndani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha