Lugha Nyingine
Wataalam wa majadiliano?wa Afrika wakutana nchini Kenya kuandaa msimamo wa pamoja kabla ya mkutano wa mabadiliko ya tabianchi
Wataalam wa majadiliano ya kufikia makubaliano zaidi ya 100 wa Afrika wameanza mkutano wa siku nne jijini Nairobi, Kenya jana Jumanne, kuandaa mpango wa awali kabla ya Mkutano wa 29 wa Nchi Watiasaini kwenye Makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) utakaofanyika Baku, Azerbaijan, mwezi Novemba mwaka huu.
Kiongozi wa Timu ya Kundi la Wataalamu Wa Majadiliano wa Afrika (AGNES) George Wamukoya amesema, wataalam hao wanatathmini machaguo na kuandaa msimamo wa pamoja wa Afrika kabla ya mkutano huo wa COP29.
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Emile Guirieoulou kutoka nchini Cote d’Ivoire amesema, wabunge wameunga mkono hatua zenye matokeo halisi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika kupitia kutunga sera na kanuni sahihi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma