Lugha Nyingine
Tukio?la Msimu?wa Kimataifa?wa Matumizi wa China na Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) Mwaka 2024 lazinduliwa
Picha ikionyesha muonekano wa shughuli hiyo. (Picha kutoka waandaaji wa shughuli hiyo)
Shuguhli ya utangazaji yenye mada ya ushirikiano wazi wa biashara ya mtandaoni wa China na Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) Mwaka 2024 kando mwa Njia ya Hariri imefanyika katika Mji wa Nanning, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, China, Tarehe 24, Septemba ambapo Tukio la Msimu wa Kimataifa wa Matumizi wa China na ASEAN Mwaka 2024 limezinduliwa rasmi.
Tukio hilo la matumizi kwenye manunuzi litadumu kwa miezi miwili ya Septemba hadi Oktoba, likiwa limegawanyika katika sehemu tano: Ulipaji kwa urahisi na matumizi””manunuzi ya bidhaa bora kwa bei nafuu””kujipatia na kutumia vyombo vipya vya nyumbani””kuonja vyakula vitamu kwa furaha”na ”kununua bidhaa maalum za Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki kwa bei nafuu”.
Tukio hilo litazindua zaidi ya shughuli 500 za kunadi bidhaa za matumizi, kama vile Gulio la Manunuzi ya Vitu Vizuri vya ASEAN Mtandaoni, kuwezesha muunganisho wa uzalishaji na uuzaji, mabadilishano na ushirikiano katika bidhaa na huduma nzuri za duniani, kupanua usambazaji wa soko la ndani kwa rasilimali za bidhaa za kimataifa, na kuhamasisha uboreshaji wa matumizi na uwezekano wa utoaji wa bidhaa mpya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma