超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

AU yaeleza wasiwasi juu ya kudhoofika kwa usalama na hali ya kibinadamu nchini Sudan

(CRI Online) Septemba 26, 2024

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat ameeleza wasiwasi wake kuhusu kudhoofika kwa usalama na hali ya kibinadamu nchini Sudan.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumanne wiki hii, Bw. Mahamat ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu hali mbaya ya usalama na kibinadamu nchini Sudan, hususan hali ilivyo katika mji wa El Fasher mkoani Darfur.

Bw. Mahamat amelaani kuongezeka kwa mapigano na mgogoro katika siku za karibuni, na kutoa wito wa kusimamishwa mara moja kwa mapigani nchini Sudan.

Pia amerejea tena imani ya Umoja wa Afrika, kwamba hakuna suluhu ya kijeshi katika mgogoro wa nchini Sudan, na kuongeza kuwa, mapigano hayo yanayoendelea yanaongeza mateso kwa Wasudan na uharibifu mkubwa kwa nchi hiyo baada ya miongo kadhaa ya mapigano na watu kulazimishwa kukimbia makazi yao.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha