超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

China yatangaza?zana ya kwanza ya sera ya mambo ya fedha kuunga mkono soko la mitaji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2024

Picha hii iliyopigwa tarehe 19 Oktoba 2023 ikionyesha Benki Kuu ya China mjini Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Peng Ziyang)

Picha hii iliyopigwa tarehe 19 Oktoba 2023 ikionyesha Benki Kuu ya China mjini Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Peng Ziyang)

BEIJING - Benki Kuu ya China imetangaza siku ya Alhamisi kuwa imeamua kuanzisha Mfumo wa Ubadilishaji kwa Kampuni za Dhamana, Mitaji na Bima (SFISF), ukiwa na kiwango cha awali cha Yuan bilioni 500 (dola kama bilioni 71 za Kimarekani) kwa ajili ya "maendeleo mazuri na thabiti ya soko la mitaji."

SFISF, ambayo ni zana ya kwanza ya sera ya mambo ya fedha iliyoanzishwa na China kuunga mkono soko la mitaji, itawezesha kampuni stahiki za dhamana, mitaji na bima kutumia mali zao ikiwa ni pamoja na bondi, hiza za ETF na hisa katika vipengele vya Faharasa ya CSI 300 kama dhamana katika kubadilishana kwa mali zenye ukwasi mwingi kama vile bondi za serikali na bili za benki kuu, Benki Kuu ya China imesema katika taarifa.

Zana hii inaweza kuboresha kwa kiasi kikubwa uwezo wa taasisi husika kupata fedha na kuwekeza kwenye soko la hisa, amesema Tian Liang, mchambuzi katika Kampuni ya Dhamana ya CITIC.

Kiwango cha SFISF kinaweza kupanuliwa kulingana na maendeleo ya hali, benki kuu hiyo imesema.

SFISF itaendeleza uwekezaji wa mtaji wa muda wa kati na mrefu na kuimarisha utulivu wa ndani sokoni, amesema Dong Ximiao, mtafiti mkuu katika Kampuni ya Matumizi ya Mambo ya Fedha ya Merchants Union.

Kuanzia Alhamisi, maombi kutoka kwa kampuni stahiki za dhamana, mitaji na bima yatakubaliwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha