Lugha Nyingine
Msichana wa Russia: Hatimaye ninaelewa kwa nini baadhi ya watu wanafikiri ninatoka Xinjiang
Katika Kivutio cha Watalii cha Mapango ya Maelfu ya Buddha cha Bezeklik, katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, China mzee mmoja alikuwa akicheza na kuimba kwa kutumia Rawap, aina moja ya ala ya muziki ya kijadi. Lina, msichana wa Russia ambaye alikuwa akishiriki katika tukio la ziara ya Xinjiang ya waandishi bora ya "Watu Elfu Kumi Kuzungumza kuhusu Xinjiang", alichukua ngoma ya mkononi kando yake na kuanza kucheza naye.
Msichana huyo wa Russia anayeweza kuongea Lugha ya Kichina kwa ufasaha amekuwa akijifunza Kichina kwa karibu miaka kumi. Leo hii, ni mtangazaji wa "Kizazi cha Sauti Mpya za Nchi za Nje" cha Chuo Kikuu cha Huaqiao, na amedhamiria kusambaza hisia zake na kile anachokiona nchini China kwa hadhira za ng'ambo kupitia video na picha, akiwaambia China ya kweli, ya pande zote na jumuishi.
Lina akirekodiwa video kwenye Kivutio cha Watalii cha Karez huko Turpan, Mkoa wa Xinjiang. (Picha na Zeng Shurou/People’s Daily Online)
Jambo ambalo limekuwa likimchanganya Lina muda wote ni kwa nini Wachina wengi walidhani kwamba anatoka Xinjiang wakati waliposikia anazungumza Kichina vizuri. Swali hilo limepata jibu baada ya kufika Xinjiang - katika Gulio Kubwa la Kimataifa la Urumqi, watu wenye mwonekano wenye kufanana kama Lina wanaweza kuonekana kila mahali. "Katika siku ya kwanza nikiwa Xinjiang, nilipata uelewa wazi zaidi wa dhana ya umoja katika utofauti wa makabila ya China," Lina amesema.
Lina amesema: “Nimekuwa muda wote ninajua mandhari ya Xinjiang ni ya kupendeza sana. Leo nimeona Mlima Huoyan. Nimejawa na matarajio kwa aina gani ya mandhari nzuri ninaweza kuona na aina gani ya desturi na utamaduni wa kienyeji nitaweza kuhisi na kujionea katika siku chache zijazo. "
Lina akitembelea Jumba la Makumbusho la Turpan. (Picha na Liu Yanxi/People’s Daily Online)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma