超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Makubaliano ya Miradi ya Utalii wa Kitamaduni yenye Thamani ya Dola Bilioni 7.2 za Kimarekani Yatiwa Saini Katikati mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 14, 2024

Watu wakitazama onyesho kwenye eneo la kivutio cha utalii katika  Wilaya ya Zhuxi ya Mji wa Shiyan, Mkoa wa Hubei, Katikati mwa China, Oktoba 12, 2024. (Xinhua/Wu Zhizun)

Watu wakitazama onyesho kwenye eneo la kivutio cha utalii katika Wilaya ya Zhuxi ya Mji wa Shiyan, Mkoa wa Hubei, Katikati mwa China, Oktoba 12, 2024. (Xinhua/Wu Zhizun)

WUHAN – Kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa utalii wa kimataifa uliofanyika jana Jumapili, Makubaliano ya miradi hamsini ya utalii wa kitamaduni yalitiwa saini, ambayo yalifikia thamani ya jumla ya yuan bilioni 51 (dola kama bilioni 7.2 za Kimarekani) katika Mkoa wa Hubei katikati mwa China.

Mashirika ya utalii ya miji mikubwa yenye vivutio vya utalii ya China na nchi na maeneo karibu 30 ambayo ni vyanzo muhimu vya watalii wanaoingia China, pamoja na viongozi wa makundi muhimu ya utalii ya ndani, walihudhuria mkutano huo, ukilenga kuongeza kasi ya ufufukaji wa shughuli za utalii za kuvutia watalii wa kimataifa nchini China na kuufanya Mkoa wa Hubei kuwa eneo la kuwavutia watalii la kiwango cha kimataifa.

Kwenye mkutano huo, maeneo ya miji 17 ya ngazi ya mikoa yametia saini makubaliano ya miradi 50 ya utalii wa kitamaduni yenye thamani ya jumla ya uwekezaji inayokadiriwa kufikia yuan bilioni 59.5.

Mkoa wa Hubei pia umezindua njia tano za usafiri wa ndege wa kutoa huduma za kipekee kwa watalii wa kimataifa wakati wa kufanyika kwa mkutano huo, njia hizo tano za usafiri wa ndege zinahusisha utalii kwenye Eneo lake maarufu la Mali ya Urithi ya Dunia la Shennongjia, Mlima Wudang na Magenge Matatu ya Mto Changjiang.

Ukiwa na mada ya kuendeleza utalii wa kuvuka mpaka na kuhimiza hali ya kufundishana kati ya watu wa nchi zenye ustaarabu tofauti, Mkutano huo wa Mwaka 2024 wa wafanyabiashara wa shughuli za utalii wa kimataifa huko Hubei umeandaliwa na idara ya utamaduni na utalii ya Mkoa wa Hubei na serikali ya Mji wa Shiyan, ukivutia washiriki zaidi ya 300.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha