Lugha Nyingine
China ingependa?kuimarisha kuendana kwa mikakati ya maendeleo na Vietnam - Waziri Mkuu wa China
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh mjini Hanoi, Vietnam, Oktoba 13, 2024. (Xinhua/Liu Weibing)
HANOI - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema jana Jumapili kwamba China ingependa kuimarisha kuendana kwa mikakati ya maendeleo na Vietnam, kutekeleza mpango wa kuunganisha Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na mkakati wa Kiuchumi wa “Shoroba Mbili na Mzunguko Mmoja” wa Vietnam.
China na Vietnam zote ni nchi zinazoendelea ambazo ziko katika hatua muhimu ya juhudi zao za ujenzi wa mambo ya kisasa, Li amesema wakati akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh, akiongeza kuwa China inaiunga mkono kithabiti Vietnam katika kufuata njia ya ujamaa inayoendana na hali yake ya kitaifa.
Li amesisitiza dhamira ya China ya kuboresha na kupandisha hadhi kila wakati ushirikiano katika sekta mbalimbali na Vietnam.
China ingependa kuzidisha ushirikiano na Vietnam katika nyanja kama vile mafungamano ya mawasiliano, biashara, uwekezaji, utalii, huduma za afya, kuzuia na kupunguza athari za maafa, vilevile kupanua ushirikiano katika kufanya malipo kwa kutumia sarafu za nchi zao na viwanda vinavyoibukia, ikiwa ni pamoja na uchumi wa kidijitali na maendeleo ya kijani, amesema.
Mwezi Agosti, Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), alifanya mazungumzo na Rais To Lam wa Vietnam ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV), wakiweka dira na kuingiza nguvu mpya kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Vietnam, Li amesema.
Amesema China ina nia ya kushirikiana na Vietnam kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa vyama na nchi hizo mbili, kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu, na kujenga hali ya kuaminiana kila wakati.
Kwa upande wake Pham, amesema Vietnam na China zinafurahia uhusiano wa karibu wa makomredi na ndugu, na kwamba urafiki wao wa jadi unazidi kuimarika.
Kuendeleza uhusiano na China ni kipaumbele cha juu na chaguo la kimkakati kwa chama na serikali ya Vietnam, Pham amesema, akiongeza kuwa Vietnam inafuata kanuni ya kuwepo kwa China moja, inaunga mkono maendeleo na ukuaji wa China, pamoja na mfululizo wa mapendekezo ya kimataifa yaliyotolewa na Rais Xi.?
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh mjini Hanoi, Vietnam, Oktoba 13, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma