Lugha Nyingine
Watu 19 wauawa katika shambulizi la Israel dhidi ya shule katika Ukanda wa Gaza
(CRI Online) Oktoba 14, 2024
Watu zaidi ya 19 wameuawa kwenye shambulizi la jeshi la Israel katika shule moja iliyoko kwenye kambi ya wakimbizi katika Ukanda wa Gaza.
Ripoti imesema, jeshi la Israel pia limeshambulia kambi nyingine ya wakimbizi kaskazini mwa Gaza na kusababisha vifo vya watoto watano.
Taarifa iliyotolewa jana Jumapili na jeshi la Israel imesema, jeshi hilo limeendelea kufanya operesheni ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza na kushambulia vituo 40 na kuua wapiganaji kadhaa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma