Lugha Nyingine
Mkoa wa Shanxi wa China washuhudia zaidi ya nusu ya makaa ya mawe yakizalishwa kwa uchimbaji wa kutumia AI
Mfanyakazi akifanya kazi katika kituo cha kuelekeza mitambo cha Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Huayang Na. 2 katika Mji wa Yangquan, Mkoa wa Shanxi, Kaskazini mwa China, Agosti 1, 2024. (Xinhua/Li Xin)
TAIYUAN - Mkoa wa Shanxi unaoongoza uzalishaji wa makaa ya mawe nchini China hivi sasa asilimia zaidi ya 50 ya uwezo wake wa kuzalisha makaa ya mawe ukifanyika kupitia uchimbaji wa kutumia akili mnemba (AI), zimesema serikali ya mkoa huo siku ya Jumatatu.
Habari zilizotolewa kwenye Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana kuhusu maendeleo ya hivi sasa ya mkoa huo kuhimiza kazi ya kubadilisha muundo wa nishati zimesema kuwa, Migodi ya makaa ya mawe ya majaribio na migodi ya vielelezo jumla ya 30 ya kufanya uzoefu wa kuchimba makaa ya mawe kwa teknolojia za kijani imeanzishwa katika mkoa mzima.
Huku karibu asilimia 82 ya uwezo wake wa kuzalisha makaa ya mawe ukiwa umeboreshwa na kutambuliwa kama uwezo wa hali ya juu, mkoa huo umedumisha uongozi wake katika uzalishaji wa makaa ya mawe nchini China kwa miaka minne mfululizo, amesema Zhang Xiang, naibu mkuu wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya mkoa huo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari.
Katika miaka mingi iliyopita, Shanxi imekuwa ikiboresha viwanda vyake vya makaa ya mawe. Mwaka 2023, mkoa huo ulianzisha migodi 118 ya makaa ya mawe ya teknolojia za AI na kuingiza teknolojia za kisasa kutumika kwenye sehemu 1,491 za uchimbaji. Hadi kufikia Mwaka 2025, migodi yote mikubwa na yenye hatari kubwa ya makaa ya mawe katika mkoa huo inatazamiwa kuwa itakamilisha mageuzi kwa teknolojia ya AI.
Mwaka 2023, Shanxi ilizalisha makaa ya mawe kwa tani zaidi ya bilioni 1.37, na imeweka lengo la uzalishaji makaa ya mawe kwa tani bilioni 1.3 kwa mwaka huu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma