Lugha Nyingine
Kituo cha Habari cha Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa kutoka nje ya China (CIIE) chafunguliwa rasmi (7)
Waandishi wa habari wanaofanya kazi katika eneo la umma la kazi ya vyombo vya habari la Kituo cha Habari. (Picha na Weng Qiyu/People's Daily Online) |
Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji bidhaa ya China CIIE yamefanyika mjini Shanghai kuanzia tarehe 5 hadi 10 Novemba. Kituo cha Habari cha CIIE kilifunguliwa rasmi tarehe 3 Novemba kwa waandishi wa habari wa nchini na nchi za nje na kitatoa huduma bora kwa karibu waandishi 3,800.
Kituo cha Habari cha CIIE kimeweka eneo la huduma ya mashauriano, eneo la umma la kazi ya vyombo vya habari, eneo maalum la kazi ya vyombo vya habari, eneo la huduma ya kiufundi ya redio na televisheni, chumba cha mahojiano, ukumbi wa mikutano na waandishi wa habari, na eneo la maonyesho ya kitamaduni, sehemu ya mapumziko ya kunywa chai na kulia chakula na maeneo mengine. Wakati wa CIIE, karibu mahojiano 50 ndani na nje ya tukio yatafanyika hapa. Vile vile, waandishi wa habari wanaweza pia kufurahia mandhari ya Mji wa Shanghai bila kutoka nje, kupata uzoefu wa vyakula maalum vya Shanghai, na miradi ya urithi wa kitamaduni usioshikika wa mtindo wa Shanghai.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma