Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping asifu mafanikio ya Macao kabla ya jubilee ya miaka 25 tangu Macao irudi China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), na mkewe Peng Liyuan wakitoka nje ya ndege na kusalimia watu waliowakaribisha huko Macao, kusini mwa China, Desemba 18, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)
MACAO - Rais wa China Xi Jinping amewasili Macao Jumatano alasiri kuhudhuria mkutano wa kuadhimisha miaka 25 tangu Macao kurudi katika nchi ya China na hafla ya kuapishwa kwa serikali ya awamu ya sita ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao (SAR) siku ya Ijumaa, ambapo amesema Macao ni kama "lulu kwenye kiganja" cha nchi mama, na kujaa imani kwa mustakabali wa maendeelo ya taifa lake China.
Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), pia atafanya ziara ya kukagua Macao.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Macao, bendi ya kikosi cha polisi cha Macao ilipiga muziki za makaribisho. Ngoma za dragoni na simba zilijaza hewa kwa furaha. Mamia ya watu wakiwemo watoto na wajumbe kutoka sekta mbalimbali walipeperusha bendera ya taifa, bendera ya Macao na maua, wakionyesha makaribisho yao kwa furaha kubwa.
Majira ya saa kumi jioni (kwa saa za Beijing), Rais Xi na mkewe Peng Liyuan, walitoka nje ya ndege maalum iliyowabeba na kupunga mkono kwa watu waliowakaribisha kwa fuhara.
"Kila ziara katika sehemu hii yenye kupendeza imekuwa ya furaha kubwa kwangu," Rais Xi amesema katika hotuba fupi kwenye uwanja wa ndege.
Katika miaka 25 iliyopita, uzoefu wa "nchi moja, mifumo miwili" wenye umaalum wa Macao umepata mafanikio yanayotambuliwa zaidi duniani, ukionyesha uhai na haiba kubwa ya kipekee, Rais Xi amesema.
"Hii ni fahari ya wakazi wa Macao na pia ni majivuno ya watu wote wa China," amesema.
Kwa niaba ya serikali kuu na watu wa makabila yote ya China, ametoa salamu za dhati na salamu za kutakia kila la kheri kwa wakazi wote wa Macao, akiongeza kuwa anafurahia muda wote maendeleo ya Macao na ustawi wa wakazi wa Macao.
Rais Xi amesema atakuwa na mazungumzo mapana na ya kina na marafiki mkoani Macao juu ya maendeleo ya mkoa huo wakati wa ziara yake hiyo.
Ameelezea imani yake kwamba Macao itajenga mustakabali mzuri zaidi kwa kutumia vya kutosha nguvu zake bora za utaratibu wa "nchi moja, mifumo miwili," kufanya kazi kwa bidii na kuhimiza uvumbuzi kwa juhudi kubwa.
Macao imejaa hali ya furaha na shamrashamra nyingi siku chache kabla ya kuadhimisha miaka 25 tangu kurejea kwake kwa nchi ya China. Mabango na mapambo ya maua ya maadhimisho vimepamba maeneo maarufu kama vile Magofu ya St. Paul's, huku bendera ya taifa na bendera ya Macao zikipepea mitaani humo.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), na mkewe Peng Liyuan wakitoka nje ya ndege na kusalimia watu waliowakaribisha huko Macao, kusini mwa China, Desemba 18, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), na mkewe Peng Liyuan wakisalimia watu waliowakaribisha huko Macao, kusini mwa China, Desemba 18, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), na mkewe Peng Liyuan wakisalimia watu waliowakaribisha huko Macao, kusini mwa China, Desemba 18, 2024. (Xinhua/Ju Peng)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba fupi kwenye uwanja wa ndege wa Macao, kusini mwa China, Desemba 18, 2024. (Xinhua/Yan Yan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma