超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Kuibuka?kwa manowari ya kwanza ya kubeba ndege za kivita inayoundwa?nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2024
Kuibuka?kwa manowari ya kwanza ya kubeba ndege za kivita inayoundwa?nchini China
Picha hii iliyopigwa Aprili 9, 2023 ikionyesha ndege ya kivita ya J-15 ikiwa tayari kuruka kutoka kwenye manowari ya kubeba ndege za kivita Shandong wakati wa doria na mazoezi ya kijeshi kuzunguka Kisiwa cha Taiwan yaliyofanywa na Kamandi ya Kivita ya Mashariki ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA). (Picha na An Ni/Xinhua)

BEIJING – Manowari ya kwanza ya kubeba ndege za kivita inayoundwa nchini China, Shandong, imeondoka kutoka kwenye gati kwa ajili ya mazoezi yake ya mwisho ya baharini mwaka 2024, katika bandari ya jeshi la majini mjini Sanya, Hainan, mkoa wa kisiwa wa kusini kabisa mwa China.

Miaka mitano iliyopita, Desemba 17, 2019, Manowari Shandong ilikabidhiwa rasmi kwa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), ikionyesha China kuingia zama ya kuwa na manowari mbili za kubeba ndege za kivita.

Ikiwa imepewa jina la Mkoa wa Shandong, ni manowari ya pili ya China ya kubeba ndege za kivita, kufuatia ile ya Liaoning, manowari iliyotengenezwa upya na manowari ya Umoja wa Kisovieti ambayo ilizinduliwa mwaka 2012.

Tangu ilipoanza kufanya kazi kikamilifu, Manowari Shandong imejumuishwa kwa haraka katika operesheni za pamoja na mifumo ya mapigano ya masafa marefu ya baharini, huku uwezo wa kivita wa kundi la manowari hiyo ukiendelea kuongezeka kwa kasi.

"Ufanisi wa pamoja wa kundi la manowari hiyo ni muhimu kwa nguvu yake ya mapigano," kamanda wa Shandong amesema.

Hiyo ilidhihirishwa mwezi Aprili 2023, wakati Kamandi ya Kivita ya Mashariki ya PLA ilipozindua doria na mazoezi ya kijeshi kuzunguka Kisiwa cha Taiwan.

Kama nguvu muhimu kwa ajili ya operesheni za masafa marefu, Manowari Shandong bado iko tayari kuzuia vitisho kutoka mbali wakati wa amani na kushambulia kwa nguvu wakati wa vita, kamada huyo amesema.

Manowari hiyo Shandong imeweka rekodi mpya za kupaa na kutua kwa ndege mfululizo.

China ilizindua manowari yake ya tatu ya kubeba ndege za kivita, Fujian, Juni 2022. Chombo hicho, kilichopewa jina la Mkoa wa Fujian, ni chombo cha kwanza cha kubeba ndege za kivita chenye kifaa cha catapult nchini China. Ikiwa na uwezo wa kubeba tani zaidi ya 80,000, Manowari Fujian ina sehemu ya kutua ndege yenye kifaa cha catapult cha sumakuumeme na gia ya kukamata.

Manowari Fujian ilikamilisha majaribio yake ya kwanza ya baharini mwezi Mei 2024, huku majaribio zaidi yakipangwa wakati ambapo ujenzi wake unaendelea.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha