超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Tanzania yaanzisha vituo 17 vya Kiswahili nje ya nchi ili kueneza lugha hiyo duniani kote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2024

DAR ES SALAAM - Tanzania imeanzisha vituo 17 vya mafunzo ya Lugha ya Kiswahili nje ya nchi ili kueneza matumizi ya lugha hiyo duniani kote, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Palamagamba Kabudi ametangaza jana Jumatano.

Kabudi amesema pamoja na kuanzisha vituo hivyo 17 vya mafunzo ya Lugha ya Kiswahili nje ya nchi, Serikali pia imejenga vituo 30 vya mafunzo nchini humo.

Waziri Kabudi akiendesha kongamano la siku moja kuhusu utamaduni wa Afrika mkoani Morogoro, mashariki mwa Tanzania, amesema vituo hivyo vimeundwa kwa mwongozo wa Baraza la Kiswahili la Taifa la Tanzania (BAKITA).

Mratibu wa kongamano hilo lililoandaliwa kwa pamoja na taasisi za ndani na nje ya nchi hiyo, Anna Tibaijuka, amesema ufundishaji wa Kiswahili unapaswa kwenda sanjari na kuhifadhi lugha za asili zaidi ya 100 nchini humo.

Takwimu zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) zimeonesha kuwa, lugha ya Kiswahili ni moja kati ya lugha 10 zinazozungumzwa na watu wengi zaidi duniani, ikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 200.

Mwaka 2021, Mkutano Mkuu wa UNESCO uliitangaza Julai 7 ya kila mwaka kuwa Siku ya Lugha ya Kiswahili ya Dunia , ikiifanya kuwa lugha ya kwanza ya Afrika kutambuliwa kwa njia hiyo na Umoja wa Mataifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha