Lugha Nyingine
Mke wa rais wa China Bi. Peng Liyuan atembelea Jumba la Makumbusho la Macao
Mke wa rais wa China Bi. Peng Liyuan ametembelea Jumba la Makumbusho la Macao tarehe 19 Desemba akiambatana na mke wa ofisa mtendaji mkuu wa Mkoa wa utawala maalumu wa Macao Bi. Zheng Suzhen.
Bi. Peng ametazama kwa makini vitu vya mabaki ya kale vilivyohifadhiwa katika jumba hilo na kupata ufahamu wa kina kuhusu mabadiliko katika historia ya Macao na hali za mkoa huo kuhusu maisha, utamaduni, viwanda, usanifu wa majengo na menginezo, na pia amekuwa na mawasiliano ya kirafiki na warithi wa utamaduni usioshikika kama vile uchoraji picha kwenye vigae vya kauri na uchongaji wa mbao.
Katika ukumbi wa ghorofa ya tatu ya jumba hilo, Bi. Peng Liyuan alizungumza na watoto waliotembelea maonyesho hayo, na kutembelea maonyesho ya bidhaa za utamaduni na ubunifu akishiriki kwenye utengenezaji wa biskuti ya lozi. Bi. Peng Liyuan aliwataka watoto hao kurithi utamaduni bora wa jadi, kuwa na upendo kwa Macao na wazalendo wa taifa, kusoma kwa bidii ili kuchangia katika ujenzi wa Macao na maendeleo ya taifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma