Lugha Nyingine
Chombo cha “Jiaolong” cha China chamaliza kazi ya mara ya 300 ya kuzamia chini baharini (4)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 19, 2024
Tarehe 18, Agosti, chombo cha “Jiaolong” kikiingia majini kwenye eneo la Bahari ya Pasifiki ya Magharibi. (Picha na Wang Yuhao/Xinhua) |
Tarehe 18, Agosti, Timu ya Utafiti wa Kisayansi ya Kimataifa ya Bahari ya Pasifiki ya Magharibi ya mwaka 2024 ilikamilisha kwa mafanikio kazi yake ya kwanza ya kuzama baharini katika safari hiyo kwenye eneo la Bahari ya Pasifiki ya Magharibi. Hii pia ilikuwa mara ya 300 ya kufanya kazi ya kuzamia chini ya bahari kwa "Jiaolong," chombo cha kwanza cha kubeba binadamu chenye uwezo wa kuzamia chini ya bahari kwa mita 7,000, chombo hicho ambacho kilichosanifiwa na kuundwa na China yenyewe.
Baada ya kupitia vipindi vya majaribio ya baharini, matumizi ya majaribio, uendeshaji wa kibiashara n.k., "Jiaolong" imeacha nyayo zake katika Bahari ya Pasifiki, Bahari ya Hindi, na Bahari ya Atlantiki.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma