Lugha Nyingine
Simulizi za Picha: Mtanzania mwenye moyo mwema wa kuwasaidia wengine anayeishi Wuhan, China (7)
Tarehe 31, Mei, Abu akiongea na watoto kwenye shughuli ya huduma ya kujitolea. |
Mtanzania Abu anasoma shahada ya uzamivu kwenye Chuo Kikuu cha Ualimu cha Huazhong cha Wuhan. Wakati wa baada ya masomo chuoni, Abu pia ni kiongozi wa timu ya wahudumu wa kujitolea ya chuo kikuu hicho inayoitwa “wanafunzi wageni walivyo kama Lei Feng”. Lei Feng alikuwa mtu aliyesifiwa sana nchini China kutokana na moyo wake wema wa kuwasaidia wengine kila mara.
Abu alivutiwa sana na utamaduni wa China aliposoma katika chuo kikuu nchini Tanzania. Mnamo mwaka 2017, alitiwa moyo na mwalimu wa Chuo cha Confucius na kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Huazhong kusoma lugha ya Kichina. Wakati Abu alipofika chuo kikuu hicho cha Wuhan, alimaliza kirahisi utaratibu wa kujiandikisha kwa msaada wa wahudumu wa kujitolea. Abu alisema, “Wahudumu hao wa kujitolea walinisaidia, na mimi pia ninatarajia kujiunga nao na kuwasaidia watu wengi zaidi.”
Baada ya kuishi kwa miaka saba mjini Wuhan, Abu amechukulia mji huo kama maskani yake ya pili. Alipoulizwa kuhusu maisha ya siku za baadaye, Abu alisema, “Ninatumai kuwa baada ya kuhitimu masomo nitaweza kubaki hapa Wuhan. Kama nikishindwa, nitarudi Tanzania na kutoa mchango wangu kwa ajili ya ushirikiano kati ya nchi mbili Tanzania na China.”
Kabla ya kuhitimu masomo, Abu na wenzake wataendelea kutoa urafiki na wema kwa watu wengi zaidi wanaohitaji msaada.
(Picha na Hu Jingwen/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma