Lugha Nyingine
Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China yaonyesha teknolojia za kuleta mapinduzi katika huduma za kiumma
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 14, 2024
Watembeleaji wa maonyesho wakitazama miundo mifano ya treni za mwendokasi kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China, Septemba 13, 2024. (People’s Daily Online) |
BEIJING - Kuanzia roboti za kutoa huduma mbalimbali kama vile kuandaa na kuhudumia watu kahawa, vifaa vya uhalisia pepe (VR) hadi vyombo vya usafiri vinavyojiendesha bila rubani au dereva, Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China Mwaka 2024 yanaonesha teknolojia ambazo zinaleta mapinduzi juu ya namna ya kutoa huduma na kuleta ufanisi na tija katika maisha ya watu.
Maonyesho hayo yaliyoanza Septemba 12 siku ya Alhamisi yakiwa na kaulimbiu ya “Huduma za Kimataifa, Kunufaika Pamoja” yamepangwa kumalizika Jumapili, Septemba 16.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma