Lugha Nyingine
Peng Liyuan ashiriki shughuli ya mawasiliano ya kitamaduni na michezo ya vijana wa China na Marekani (2)
BEIJING - Peng Liyuan, mke wa Rais wa China Xi Jinping, ameshiriki kwenye shughuli ya mawasilliano ya kitamaduni na michezo ya vijana wa China na Marekani katika Shule ya Sekondari Na. 8 ya Beijing siku ya Jumanne adhuhuri ambapo kwenye shughuli hiyo, alifanya mazungumzo mazuri na ujumbe wa vijana hao kutoka Jimbo la Washington nchini Marekani.
Amekaribisha walimu na wanafunzi kutembelea China, akielezea matumaini kwamba vijana wa nchi hizo mbili watafahamiana zaidi na kuingiza nguvu katika uhusiano wa pande mbili.
Peng alitazama mechi ya kirafiki kati ya timu za mpira wa kikapu za vijana za China na Marekani na kutoa medali za ukumbusho kwa wachezaji wa pande zote mbili.
Peng pia alitazama video inayoonesha ziara ya ujumbe wa vijana hao katika maeneo mbalimbali nchini China. Wajumbe wa wanafunzi hao wa Marekani wameelezea mambo waliyojionea yasiyosahaulika kwenye ziara hiyo, ambayo yamewasaidia kupata ufahamu zaidi kuhusu desturi tofauti za kikabila na utamaduni mzuri wa kijadi wa China.
Ziara hiyo ina mambo mengi na ya kupendeza, inasaidia kuendeleza urafiki wa kina kati ya wanafunzi wa Marekani na wenzao wa China, na hakika itaacha kumbukumbu zaidi kwa kila mtu, Peng amesema.
Peng amesema kuwa mustakabali wa uhusiano wa China na Marekani utaamuliwa na vijana, na ameeleza matumaini yake kwamba wanafunzi wa Marekani wataelezea mambo waliyojionea kwa familia, marafiki na wanafunzi wenzao watakaporudi Marekani, kurudi nyumbani na urafiki wa watu wa China, na kusaidia kukuza "mti wa urafiki" kati ya watu wa pande hizo mbili.
Mwishoni mwa shughuli hiyo, vijana hao wa China na Marekani waliimba kwa pamoja nyimbo za lugha za Kichina na Kiingereza. Na Peng alijiunga nao na kupiga picha kwa pamoja katika hali ya ukarimu na urafiki.
Novemba Mwaka 2023, Rais Xi Jinping alitangaza mjini San Francisco mpango wa kualika vijana 50,000 wa Marekani kutembelea China kwa ajili ya programu za mawasiliano na masomo katika kipindi cha miaka mitano.
Ujumbe huo wa walimu na wanafunzi karibu 100 kutoka zaidi ya shule 10 za sekondari katika jimbo la Washington walikuja China kwa mwaliko wa Shirika la Urafiki wa Watu wa China kwa Nchi za Nje .
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma