Lugha Nyingine
Usokotaji?wa Kamba na Nyavu waendeleza?Tasnia?na Kutajirisha Watu Huko Huimin, Mkoa wa Shandong, China (3)
Mfanyakazi akitengeneza bidhaa za nyavu za Kamba katika Kampuni ya Bidhaa za Michezo ya Danlin, Mji wa Binzhou, Mkoa wa Shandong, Oktoba 8.(Xinhua/Yang Shiyao) |
Tasnia ya nyavu za kamba katika Wilaya ya Huimin, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China ina historia ya miaka zaidi ya 300. Katika miaka ya hivi karibuni, wilaya hiyo imetegemea Miji midodo ya Lizhuang na Jianglou kama msingi wa kuendeleza tasnia ya nyavu za kamba na kuchangia kuwezesha ustawi wa vijijini.
Kwa sasa, Wilaya ya Huimin imeunda mfumo mzima wa tasnia hiyo unaojumuisha ugavi wa malighafi, Utafiti, Uendelezaji na bunifu wa bidhaa, utengenezaji wa bidhaa kamili, masoko na huduma za utumaji. Pia imeteuliwa kuwa nguzo ya kampuni ndogo na za kati za tasnia maalum ya ngazi ya kitaifa.
Sehemu ya soko ya bidhaa za nyavu za kamba kutoka wilaya hiyo huchukua zaidi ya asilimia 80 ya soko zima la China na tasnia hiyo ya nyavu imekua tasnia maalum ongozi ambayo inaendeleza tasnia za kienyeji na kutajirisha watu.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma