超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

China Bara na?Hong Kong zakubaliana kuendeleza biashara ya huduma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 10, 2024
China Bara na?Hong Kong zakubaliana kuendeleza biashara ya huduma
Paul Chan, ofisa wa mambo ya fedha wa serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR), akizungumza kwenye hafla ya kutia saini nyaraka kuhusu kurekebisha makubaliano ya biashara ya huduma chini ya Mpango wa Ushirikiano wa Karibu zaidi wa Kiuchumi (CEPA) mjini Hong Kong, kusini mwa China, Oktoba 9, 2024. (Idara ya Huduma za Habari ya Serikali ya HKSAR/kupitia Xinhua)

BEIJING – China Bara na Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) zimekubaliana kujenga uhusiano wa karibu zaidi katika biashara ya huduma, Wizara ya Biashara ya China imesema siku ya Jumatano.

Li Yongsha, ofisa katika wizara hiyo, na Paul Chan, ofisa wa mambo ya fedha wa serikali ya HKSAR, wametia saini nyaraka kuhusu kurekebisha makubaliano ya biashara ya huduma chini ya Mpango wa Ushirikiano wa Karibu zaidi wa Kiuchumi (CEPA) mjini Hong Kong siku ya Jumatano.

Makubaliano hayo yataanza kufanya kazi rasmi kuanzia tarehe ya kutiwa saini na yataanza kutekelezwa rasmi kuanzia tarehe 1 Machi 2025.

Kwa mujibu wa marekebisho hayo, vigezo vya kuingia soko la China Bara kwa watoa huduma wa Hong Kong katika nyanja zikiwemo fedha, mawasiliano ya simu, usanifu majengo na utalii vitapunguzwa zaidi au kuondolewa.

Ikiwa ilitiwa saini kati ya China Bara na Hong Kong mwaka 2003, CEPA imewezesha kwa kiasi kikubwa kuzifanya biashara zote katika bidhaa na huduma kuwa huria.

Marekebisho hayo ni hatua muhimu ya kuboresha mfumokazi wa Hong Kong kutoa mchango mkubwa zaidi katika ufunguaji mlango wa China, imesema wizara hiyo, ikiongeza kuwa ni mara ya pili kwa makubaliano hayo ya biashara ya huduma ya CEPA kufanyiwa marekebisho, ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2019.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha