Lugha Nyingine
Karez, “mfereji wa chini ya ardhi” wa China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 15, 2024
Visima vya Karez ni mradi wa kipekee wa uhifadhi wa maji na umwagiliaji chini ya ardhi mkoani Xinjiang, China, ambao unajulikana kwa jina la “Ukuta Mkuu wa maji wa chini ya ardhi" na "mfereji wa chini ya ardhi”.
Ni moja kati ya miradi mikubwa mitatu ya kale ya China sambamba na Ukuta Mkuu na Mfereji Mkuu wa Beijing-Hangzhou. Uliingizwa kwenye "Orodha ya Urithi wa Uhandisi wa Umwagiliaji wa Dunia (kundi la 11) 2024" mwezi Septemba mwaka huu.
Kuna visima vya karez zaidi ya 1,700 katika mkoa wa Xinjiang, kati ya hivyo, zaidi ya 1,200 vipo katika Mji wa Turpan, vikiwa na urefu wa jumla wa kilomita 5,272.
Theluji juu ya Mlima Tianshan baada ya kuyeyuka hutiririka kupitia visima hivyo vya karez kurutubisha Turpan, ikileta uhai kwa ardhi hiyo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma