超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

DPRK yathibitisha kuzuiwa kabisa kwa mawasiliano ya barabara?na?reli kuelekea Korea?Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 17, 2024

Picha hii isiyo na tarehe iliyotolewa na Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA) ikionyesha brabara na reli ikiwa imelipuliwa nchini Korea Kaskazini (DPRK). (KCNA/ kupitia Xinhua)

Picha hii isiyo na tarehe iliyotolewa na Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA) ikionyesha brabara na reli ikiwa imelipuliwa nchini Korea Kaskazini (DPRK). (KCNA/ kupitia Xinhua)

SEOUL - Korea Kaskazini (DPRK) imesema Alhamisi kwamba barabara na reli zinazounganisha Korea Kusini (ROK) katika maeneo ya mashariki na magharibi mwa mpaka wa kusini wa DPRK zimezuiwa kabisa, Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA) limeripoti.

"Chini ya amri ya Kamati Kuu ya Kijeshi ya Chama cha Wafanyakazi wa Korea Kaskazini, Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Korea Kaskazini (KPA) tarehe 15 Oktoba alichukua hatua ya kukata barabara na reli za Korea Kaskazini ambazo zinaelekea Korea Kusini kupitia sehemu za mashariki na magharibi za mpaka wa kusini wa Korea Kaskazini kama sehemu ya kutenganisha kabisa eneo lake, kutoka kwenye eneo la Korea Kusini," KCNA imesema, ikirejelea Korea Kusini kwa kutumia kifupi cha jina lake rasmi la Jamhuri ya Korea.

"Mchana wa Oktoba 15, sehemu zenye urefu wa mita 60 za barabara na reli katika eneo la Kamho-ri, Kaunti ya Kosong, Jimbo la Kangwon na sehemu zenye urefu wa mita 60 za barabara na reli katika eneo la Tongnae-ri, Wilaya ya Panmun, Manispaa ya Kaesong zimezuiwa kabisa kwa mlipuko," msemaji wa Wizara ya Ulinzi wa Taifa ya Korea Kaskazini amenukuliwa na KCNA akisema.

"Hii ni hatua isiyoepukika na halali iliyochukuliwa kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Korea Kaskazini ambayo inaifafanua wazi Korea Kusini kuwa nchi adui, na kutokana na mazingira mabaya ya kiusalama yanayoelekea ukingoni kutokea vita kwa sababu ya uchochezi mkubwa wa kisiasa na kijeshi," ripoti hiyo ya KCNA imeeleza.

Mkuu wa Jeshi la Watu wa Korea Kaskazini (KPA) alisema Oktoba 9 kwamba nchi hiyo itakata kabisa barabara na reli zinazounganisha Korea Kusini huku kukiwa na hali ya hatari kwenye Peninsula ya Korea, ripoti ya awali ya KCNA ilisema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha