Lugha Nyingine
Kuunganishwa kwa Reli ya Ethiopia-Djibouti na eneo la biashara huria kwachochea uchumi wa Ethiopia
(CRI Online) Oktoba 18, 2024
Kampuni ya Ubia ya Reli ya SGR kati ya Ethiopia-Djibouti (EDR) imesema, kuunganishwa kwa reli ya Ethiopia-Djibouti na Eneo la Biashara Huria la Ethiopia la Dire Dawa kutachochea ukuaji wa uchumi.
Shirika la Utangazaji la Ethiopia Fana limeripoti kuwa, kuunganishwa kwa eneo hilo la biashara huria na reli hiyo kunatarajiwa kuboresha biashara katika kanda hiyo kutokana na mtandao wa usafirishaji.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa EDR Takele Uma amesema, hii ni hatua muhimu kwa miundombinu ya reli katika sehemu hiyo, na kwamba wakati reli ya Ethiopia-Djibouti inapoendelea kupanua na kuboresha huduma zake, imekuwa nguzo ya ukuaji wa uchumi katika kanda hiyo, na kuimarisha jukumu lake katika kujenga mustakabali wa uchumi wa nchi hiyo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma