Lugha Nyingine
Meli hospitali ya Kikosi cha Majini cha Jeshi la China yafanya ziara Benin kwa mara ya kwanza
(CRI Online) Oktoba 18, 2024
Meli hospitali ya Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi la China (PLA) "Peace Ark" inayotekeleza "Kazi ya Mapatano (Mission Harmony) -2024" imewasili kwenye Bandari ya Cotonou jana Alhamisi na kuanza ziara ya siku saba ya kutoa huduma za matibabu nchini Benin, ikiwa ni mara ya kwanza kwa meli hiyo kufanya ziara Benin.
Katika ziara hiyo, madaktari wa China watatoa huduma za matibabu katika meli hiyo na kupeleka timu ya matibabu katika vituo vya vijana na vyuo vikuu vya huko kwa lengo la kutoa matibabu na kubadilishana uzoefu na madaktari wa huko.
Madaktari wa jeshi la Benin waliopata mafunzo nchini China watatembelea meli hiyo na kufanya mazungumzo ya kina na wataalam wa matibabu wa China.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma