Lugha Nyingine
Sudan na Sudan Kusini zajadili kurejesha usafirishaji wa mafuta
Sudan na Sudan Kusini zimesisitiza haja ya kushughulikia vikwazo vinavyokabili urejeshwaji wa shughuli za usafirishaji wa mafuta ya Sudan Kusini kupitia ardhi ya Sudan.
Hii imefahamika baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Mamlaka ya Mpito la Sudan na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sudan (SAF) Abdel Fattah Al-Burhan kukutana na Mshauri wa Usalama wa Taifa Rais wa Sudan Kusini Bw. Tut Gatluak mjini Port Sudan, Mashariki mwa Sudan.
Akionesha utayari wa kutekeleza mambo waliyojadili, Bw. Gatluak amesema timu zote za kiufundi katika nchi hizo mbili ziko tayari kuongeza uzalishaji na kuhakikisha usafirishaji wa mafuta kupitia bandari ya Bashayer ya Sudan.
Habari pia zinasema mkutano kati ya wizara za nishati na mafuta za nchi hizo mbili unatarajiwa kufanyika ili kufanikisha jambo hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma