Lugha Nyingine
Sudan yakubali kufungua viwanja?vingine?vinne vya ndege kwa mashirika ya kibinadamu
KHARTOUM - Serikali ya Sudan imesema imekubali kufungua viwanja vingine vinne vya ndege kwa mashirika ya kibinadamu ili kupeleka misaada katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita, Baraza la Mamlaka ya Mpito la Sudan limesema siku ya Jumamosi.
Viwanja vya ndege vitakavyofunguliwa viko katika miji ya Kassala, Dongola, El Obeid na Kadugli, taarifa iliyotolewa na baraza hilo imesema.
Kupitia hatua hiyo, "serikali ya Sudan imetimiza mahitaji yote ya kuingia na kusambazwa kwa misaada ya kibinadamu kwa njia ya anga, nchi kavu na baharini," imesema taarifa hiyo, ikiongeza kuwa sasa kuna viwanja sita vya ndege na vivuko saba vya nchi kavu vinavyopatikana kwa mashirika ya kimataifa.
Picha hii iliyopigwa Oktoba 16, 2024 ikionyesha misaada ya kibinadamu ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Port Sudan, mashariki mwa Sudan. (Wizara ya Afya ya Sudan/kupitia Xinhua)
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, nusu ya wakazi wa Sudan, karibu watu takriban milioni 25, wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi, wakati milioni karibu 18 wanakabiliwa na hali ya ukosefu wa usalama wa chakula.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani hapo awali lilionya kuwa Sudan inaweza kukabiliwa na janga kubwa zaidi la njaa duniani wakati ambapo mgogoro huo unaingia mwaka wake wa pili.
Sudan imekuwa ikikumbwa na mgogoro mbaya kati ya Jeshi la Sudan na Vikosi vya Mwitikio wa Haraka tangu katikati ya Aprili 2023. Mgogoro huo umesababisha vifo vya takriban watu 20,000, maelfu ya majeruhi, na mamilioni ya watu kuyakimbia makazi yao, kwa mujibu wa makadirio ya hivi karibuni ya Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.
Wafanyakazi wakipakua misaada ya kibinadamu kwenye uwanja wa ndege wa Port Sudan, mashariki mwa Sudan, Oktoba 16, 2024. (Wizara ya Afya ya Sudan/kupitia Xinhua)
Wafanyakazi wakipakua misaada ya kibinadamu kwenye uwanja wa ndege wa Port Sudan, mashariki mwa Sudan, Oktoba 16, 2024. (Wizara ya Afya ya Sudan/kupitia Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma