Lugha Nyingine
Watu wenye vipaji vya usanii waingizwa kusaidia kustawisha kijiji cha kale kusini mwa China (6)
Picha hii iliyopigwa tarehe 13 Desemba 2024 ikionyesha picha ya rangi iliyochorwa kwenye ukuta wa nyumba ya zamani katika kijiji cha kale cha Hakka karibu na Kijiji cha Shangwei. (Xinhua/Wu Zhizun) |
Wanakijiji wakisoma vitabu vya katuni kwenye kituo cha watoto katika Kijiji cha Shangwei, ambacho ni kijiji cha Hakka chenye historia ya miaka ya zaidi 400, katika Eneo la Longhua la Mji wa Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Desemba 13, 2024.
Tangu Mwaka 2017, serikali ya mtaa imeingiza watu wenye vipaji vya usanii takriban 100 katika Kijiji cha Shangwei ambacho ni kijiji cha Hakka chenye historia ya miaka ya zaidi ya 400, katika Eneo la Longhua la Mji wa Shenzhen ili kusaidia kustawisha kijiji hicho cha kale kwenye msingi wa kutumia sanaa ya uasili na ubunifu wa kitamaduni.
Kijiji hicho bado kinahifadhi nyumba tano za ulinzi za Diaolou zilizojengwa zaidi ya miaka mia moja iliyopita na nyumba karibu 50 za zamani za Hakka, ambapo studio za wasanii, jumba la makumbusho, na majengo ya kufanyia maonyesho vinatapakaa kijijini humo . Shughuli mbalimbali za kitamaduni zimekuwa zikifanyika na kuvutia washiriki karibu 70,000. Kijiji hicho kimekuwa mfano hamasishi wa kitamaduni na kimeleta mabadiliko makubwa kwa vijiji vingine vya zamani vya Hakka vilivyoko karibu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma