Lugha Nyingine
Wanaanga?wa chombo cha Shenzhou-19 wakamilisha shughuli za kwanza nje ya chombo
BEIJING – Wanaanga wa chombo cha Shenzhou-19 wamekamilisha shughuli za kwanza za nje ya kituo cha anga ya juu ya China(EVAs) majira ya saa 3:57 Usiku (Saa za Beijing) jana Jumanne, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA).
Cai Xuzhe, Song Lingdong na Wang Haoze, wamefanya kazi kwa saa tisa katika kukamilisha kazi mbalimbali, zikiwemo kufunga vifaa vya kulinda vifusi kwenye anga ya juu. Wamesaidiwa na mkono wa roboti wa kituo hicho cha anga ya juu na timu iliyoko duniani.
Cai na Song, wanaanga wawili waliopewa jukumu hilo, tangu wakati huo wamerejea salama kwenye chombo cha maabara cha Wentian.
Jukumu la kazi za kwanza za nje ya chombo za wanaanga hao wa Shenzhou-19 limekuwa lenye mafanikio makubwa, ikiweka rekodi mpya ya muda mrefu wa kufanya shughuli za nje ya chombo kwa wanaanga wa China, imesema CMSA.
Hii ni mara ya pili ya Cai kwenye kufanya shughuli nje ya chombo, kufuatia safari yake ya awali wakati wa jukumu la chombo cha Shenzhou-14 miaka miwili iliyopita. Song amekua mwanaanga wa kwanza wa China aliyezaliwa baada ya 1990 kutekeleza jukumu hilo, limesema shirika hilo.
Wanaanga hao wa Shenzhou-19 wamepangwa kufanya majaribio kadhaa ya sayansi na majaribio ya kiufundi kwenye anga ya juu, pia watafanya shughuli za nje ya chombo na kufunga vifaa nje ya kituo hicho cha anga ya juu, shirika hilo limeongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma