超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Mkoa wa Henan nchini China wahimiza utalii na utamaduni ili kuvutia watalii zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2024
Mkoa wa Henan nchini China wahimiza utalii na utamaduni ili kuvutia watalii zaidi
Onyesho la moja kwa moja jukwaani la "Huan Su·Dayi Shang". (Picha na Wang Pei,People's Daily Online)

Mto Manjano ulizaa ustaarabu mzuri sana wa China. Ukipatikana katikati mwa utamaduni wa Mto Manjano, Mkoa wa Henan una rasilimali nyingi za kihistoria na kitamaduni. Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya mawazo mapya, matukio mapya na njia mpya za kucheza katika utalii wa kitamaduni wa Mto Manjano zimeibuka kimya kimya kusini mwa mto huo.

Ukiwa ni mkoa wenye idadi kubwa ya mabaki ya kitamaduni na urithi wa utamaduni usioshikika wa Mto Manjano, utalii wa kitamaduni wa Henan umekuwa hali moto moto kwa muda mrefu.

Katika miaka ya hivi karibuni, kuongezeka kwa mitindo ya kisasa maarufu ya kitaifa kumekuwa kukijitokeza, na mkoa huo wa Henan umechukua fursa hiyo. Kuanzia Januari hadi Julai mwaka huu, majumba ya makumbusho kote mkoani humo yalipokea watembeleaji zaidi ya milioni 42.6, na "kwenda kwenye majumba ya makumbusho" imekuwa mtindo mpya kwa vijana.

Huang Dongsheng, mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni na Utalii ya Mkoa wa Henan, ameeleza kwamba Henan inapanga kujenga barabara kuu No.1 ya watali ya "Mji Mkuu wa Kale wa Mto Manjano" yenye urefu wa kilomita jumla ya 4,810, na itatengeneza ushoroba wa utalii wa kitamaduni wa Mto Manjano wenye safari za watalii za "mwendo wa haraka, mwendo wa polepole, hali changamani".

Baada ya kuona "Unique Henan, Land of drama" kwenye jukwaa la kuchapisha video mtandaoni, Chen Jie alivutiwa sana na akaenda moja kwa moja hadi Zhengzhou kutazama uhalisia. Baada ya kutoka katika "Unique Henan, Land of drama", Chen Jie aliamua kutembelea Jumba la Makumbusho la Henan na maeneo mengine tena. "Henan ni hazina ya kitamaduni, yenye gharama stahiki ya kujionea kwetu."

Aidha, Henan imeanzisha "kanzidata" ya rasilimali za urithi wa kitamaduni wa Mto Manjano, imechambua miradi 947 ya urithi wa utamaduni usioshikika wa ngazi ya mkoa na zaidi, miradi muhimu 488 ya kitamaduni, na kuanzisha ushoroba wa ulinzi kwa maeneo maalum ya urithi ya kiwango cha kimataifa kando ya Mto Manjano.

Alasiri ya majira ya baridi kali, gongo na ngoma za Shanzhou huchezwa katika Eneo Maalum la Utamaduni wa Jadi la Shanzhou Dikengyuan katika Mji wa Sanmenxia. Hapo awali, urithi wa patu na ngoma daima lilikuwa jambo linalojaliwa sana na mwimbaji mkubwa wa eneo hilo, Qin Xianchou.

Kwa bahati nzuri, chini ya uongozi wa serikali, eneo hilo la Shanzhou Dikengyuan lililindwa kwa uangalifu na kujengwa kuwa mradi wa utalii wa kitamaduni. Baada ya Dikengyuan kuwa maarufu, Qin Xianchou alichukua faida ya fursa hiyo kusogeza jukwaa la patu na ngoma za Shanzhou hadi hapa, na urithi huo wa utamaduni usioshikika ambao haukuwa na umaarufu ukawa mpango maarufu.

Utamaduni wa Mto Manjano umewezesha tija mpya bora ya utalii wa kitamaduni wa Henan. Huang Dongsheng ameeleza kwamba Mkoa wa Henan utaendelea kuweka ujenzi wa Ushoroba wa Utalii wa Kitamaduni wa Mto Manjano katika nafasi muhimu, na huku kukiwa na vivutio vya kitalii vya kiwango cha juu na maeneo ya mapumziko ya watalii kama vile Mapango ya Longmen, Hekalu la Shaolin, na Mifupa ya Mwaguzi ya Yinxu yataifanya Zhengbian Luo'an kuwa kivutio maarufu cha utalii wa kitamaduni na kujitahidi kufikia kiwango cha kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha