Lugha Nyingine
Makamu Rais wa Uganda apongeza mpango wa China wa maendeleo ya kijani
KAMPALA - Makamu Rais wa Uganda Jessica Alupo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Rukia Nakadama, naibu waziri mkuu wa tatu wa Uganda, kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti yaUchumi, Jamii na Utawala Mwaka 2023-2024 ya Kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China (CCCC) Tawi la Uganda siku ya Alhamisi jioni amesema uamuzi wa China wa kushirikiana na Afrika katika kuendeleza maendeleo ya kijani unaendana na malengo ya maendeleo ya Uganda na ni nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo endelevu ya nchi yake.
Maendeleo ya kijani ni mojawapo ya hatua 10 za ushirikiano ambazo China ilitangaza katika Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliomalizika hivi karibuni mjini Beijing.
Alupo amesema Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekuwa akisisitiza dhamira ya serikali ya kuhakikisha maendeleo endelevu kwa kulinda mazingira kupitia juhudi za maendeleo zinazowajibika.
"Tunafahamu kuwa mabadiliko ya tabianchi ni tishio halisi ambalo ni lazima tukabiliane nalo, tuna furaha kuambiwa kwamba CCCC inafahamu ukweli huu. Kama kanuni zozote za mazingira, kijamii na utawala katika sehemu zenu za kazi, hii itahakikisha maendeleo endelevu," Alupo amesema.
Amesema kuwa tangu Mwaka 1996, Kampuni ya CCCC tawi la Uganda imejenga barabara za lami zenye urefu wa kilomita zaidi ya 1,000, kutoa ajira kwa wenyeji na kuchangia maendeleo ya nchi.
"Miradi hii imeleta manufaa makubwa ya kiuchumi na kijamii, na kutambuliwa na kusifiwa na serikali na watu wake. Kazi ya kampuni hii imetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi ya Uganda," amesema.
Zhang Lizhong, Balozi wa China nchini Uganda, amesema ripoti hiyo inaonyesha uwajibikaji wa kijamii wa jumuiya ya wafanyabiashara wa China katika kuunga mkono ujenzi wa miundombinu na maendeleo endelevu ya Uganda.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma