Lugha Nyingine
China yatuma kikosi cha manowari cha jeshi la majini kwenda kulinda usalama katika Ghuba ya Aden (3)
Kikosi cha manowari cha Jeshi la Majini kimefanya hafla ya kuaga kwenye bandari moja ya Mji wa Zhoushan, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Desemba 15, 2024. (Picha na Han Lin /Xinhua) |
HANGZHOU – Kikosi kipya cha manowari cha Jeshi la Majini la China jana Jumapili kimefunga safari kutoka bandari ya kijeshi ya Zhoushan, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China kwenda kutekeleza jukumu la kulinda usalama kwenye Ghuba ya Aden na eneo la baharini karibu na Somalia badala ya kikosi cha manowari kilichomaliza muda wao wa kulinda ulinzi.
Kikosi hicho cha 47 cha manowari cha Jeshi la Majini kinajumuisha manowari ya kuharibu makombora, manowari ya kufanya ulinzi kwa makombora na manowari ya ugavi. Manowari hizo zinabeba maafisa na askari zaidi ya 700, ikiwa pamoja na helikopta mbili na askari zaidi ya 10 wa kikosi maalum .
Kabla ya kuondoka, kikosi hicho kilifanya mazoezi hasa kuhusu uokoaji wa kijeshi wa meli za kibiashara zilizotekwa nyara, kukabiliana na ugaidi na kupambana na uharamia, na mazoezi ya kutumia silaha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma