超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

China yatuma kikosi cha manowari cha jeshi la majini kwenda kulinda usalama katika Ghuba ya Aden

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 16, 2024
China yatuma kikosi cha manowari cha jeshi la majini kwenda kulinda usalama katika Ghuba ya Aden
Maofisa na askari wa China wakipiga saluti kwenye bandari moja ya Mji wa Zhoushan, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Desemba 15, 2024. (Picha na Yang Jingcong /Xinhua)

HANGZHOU – Kikosi kipya cha manowari cha Jeshi la Majini la China jana Jumapili kimefunga safari kutoka bandari ya kijeshi ya Zhoushan, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China kwenda kutekeleza jukumu la kulinda usalama kwenye Ghuba ya Aden na eneo la baharini karibu na Somalia badala ya kikosi cha manowari kilichomaliza muda wao wa kulinda ulinzi.

Kikosi hicho cha 47 cha manowari cha Jeshi la Majini kinajumuisha manowari ya kuharibu makombora, manowari ya kufanya ulinzi kwa makombora na manowari ya ugavi. Manowari hizo zinabeba maafisa na askari zaidi ya 700, ikiwa pamoja na helikopta mbili na askari zaidi ya 10 wa kikosi maalum .

Kabla ya kuondoka, kikosi hicho kilifanya mazoezi hasa kuhusu uokoaji wa kijeshi wa meli za kibiashara zilizotekwa nyara, kukabiliana na ugaidi na kupambana na uharamia, na mazoezi ya kutumia silaha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha